Mlinzi wa timu ya Al Masry, Ahmed Abdulraof amesema bado Simba ina nafasi ya kufanya vizuri katika mchezo wa marudiano nchini Misri licha ya sare ya mabao 2-2.

Mlinzi huyo ambaye alifunga bao la pili la Al Masry kwa mkwaju wa penati alisema kama Simba itabidilika kidogo kwenye mchezo wa marudiano wanaweza kushinda.

Abdulraof ameiambia Dar24 kuwa Simba ina kikosi kizuri na wanategemea mchezo wa marudiano utakuwa mgumu kuliko watu wanavyodhani.

“Simba bado wana nafasi na mechi ya marudiano itakuwa ngumu tunarudi nyumbani kujiandaa kwa mchezo huo,” alisema Abdulraof.

Simba itahitaji kupata ushindi kwenye mchezo huo au sare ya kuanzia mabao matatu kitu ili kusonga mbele kitu ambacho ni kigumu.

Ethiopia waienzi Siku ya Wanawake kwa wanafunzi
Agundua ana ujauzito nusu saa kabla ya kujifungua