Kampuni ya Facebook imeshtakiwa kwa tuhuma za kuwafuatilia watumiaji wa Instagram kwa kutumia camera za simu bila ya kuwa na ridhaa kutoka kwa watumiaji.
Kwa mujibu, wa ripoti za vyombo vya habari mtandao huo umekuwa ukitumia kamera za simu aina Iphone hata pale ambapo watumiaji wa wa simu hizo hawatumii kamera.
Kesi hiyo ambayo imefunguliwa New Jersey Marekani, mtumiaji wa Instagram ambaye ni mlalamikaji Brittany Conditi, amesema kuwa program hiyo ya Facebook inatumia camera za Iphone kwa makusudi ili kukusanya taarifa za siri.
Hata hivyo kampuni hiyo imekanusha taarifa tuhuma hizo na kueleza kuwa kulikuwa na hitilafu ya programu (bug).
Aidha imesema kuwa (bug) ilikuwa ikitoa taarifa kwa watumiaji wa Instagram kuwa Iphone inatumia kamera zao jambo ambalo halikuwa kweli.
Itakumbukwa mwezi uliopita Kampuni ya Facebook, ilituhumiwa kutumia teknolojia ya utambuzi wa sura na kukusanya taarifa za watumiaji wa Instagram zaidi ya millioni 100 kinyume na sheria .