Wigi huvaaliwa zaidi na wanawake wenye asili ya Afrika au Wamarekani wa saili ya Afrika.
Chimbuko halisi la uvaaji wigi ni ubaguzi uliokuwepo wakati wa utumwa ambapo wale wenye ngozi nyeupe na nywele shombeshombe walipewa kazi za rahisi za ndani na wale wasio na ngozi nyeupe walifanyishwa kazi ngumu mashambani.
Sababu kubwa ambayo inadhaniwa kuwaathiri wanawake wa asili ya kiafrika ni fikra kuwa mwanamke mwenye nywele ndefu ndio mrembo zaidi kuliko mwanamke mwingine.
Hivyo wanawake wengi wanajaribu kuutafuta urembo huo kwa kuvaa mawigi, daktari wa mambo ya afya amebainisha baadhi ya madhara hasi yanayosababishwa na kuvaa mawigi na usukaji wa nywele za bandia.
Kupata mba, hii ni kutokana na kukosekana kwa hewa ya kutosha ya oksijeni katika ngozi ya kichwa na katika tishu za shina la nywele wasichana wengi wamekuwa wakilalamikia nywele zao kuwa na mba.
Kunyonyoka nywele na maumivu ya kichwa ya mara kwa mara kutokana na mkandamizo wa kichwa .
Harufu mbaya , upotevu wa muda na fedha , hivyo kwa mwanamke anayechagua kuvaa wigi anapaswa kuwa na matunzo makubwa na nywele zake za asili na ahakikishe ananunua yenye ubora unaotakiwa ili kuepuka madhara ya kiafya yatokanayo na wigi bandia.