Wanadamu na viumbe kwa ujumla wameumbwa kwa jinsi mbili, ambapo Mwenyezi Mungu ameumba kila kitu katika pea mbili kwa maana ya jinsia ya KE na ME na katika vitu vingi ufanisi wake upo hivyo kwa jike na dume huku watengenezaji wa vitu mbalimbali pia wameviweka katika sura hiyo baadhi ya vitu.
Wasifu wa viungo katika ufanisi, pia vinakuwa pea mbili jike na dume yaani vitu hivi lazima vitofautiane na kwani kila jambo lina sifa zake ambazo zaweza kuwa ni za kiume au za kike ingawa kwa wanadamu kuna wanawake na wanaume na kila mmoja amepewa wasifu wake.
Lakini kwa upande wa dini, yenyewe imekataza mwanaume kujifananisha na mwanamke na mwanamke kujifananisha na mwanaume na hili limethibitishwa na Sheikh Mussa Kundecha, ambaye kupitia kipindi cha Balagha cha Dar24 ameelezea umuhimu wa kutofautisha mapambo ya kike na ya kiume na madhara ya pambo la dhahabu kwa wanaume.
Sheikh Kundecha anasema kwamba, yapo mambo ya kike na yapo mambo yatakuwa ya kiume ambapo amefafanua usafi ambao unawahusu wanawake na wanaume kwa pamoja akisema, “katika uislamu mtume anasema uislamu ni usafi jisafisheni.”
Aidha, anaendelea kueleza kuwa katika Uislam “jisafisheni kwa maana zote jisafisheni kwenye mavazi yenu, kwenye miili yenu jisafisheni katika nafsi zenu ziwe safi ziwe njema ziwe na fikra njema ilo ni jambo la msingi linawahusu wanaume na wanawake.”
Kadhalika, Sheikh Kundecha amezungumzia mapambo ambapo ametofautisha ya kike na ya kiume akisema “kwa upande wa dini dhahabu nipambo la kike na fedha ni pambo la kiume ikiwa mwanadamu lazima ajipambe kwa vito na madini basi mwanaume ajipambe kwa fedha na mwanaume ajipambe kwa dhahabu kama sehemu itakayo onesha tofauti kati yao.”
Aidha ameongeza kuwa, “Kama ilivyoharamishwa mwanaume kujifananisha na mwanamke basi pia uharamu huo unakwenda mpaka kwenye vitu vilivyotengenezwa kwajili ya mapambo kwahivyo dhahabu ni mapambo ya kike fedha ni mapambo ya kiume.”
Baadhi ya mapambo, kama cheni mwanaume haruhusiwi kuvaa maana hilo ni pambo la kike kama ilivyo kwa sikio na pua ni pambo la kike pia, ingawa Kundecha anakemea tabia haramu za baadhi ya watu kuanza kuhalalisha vitu vilivyoharamishwa na Mtume na MUNGU.
Hata hivyo, inashauriwa kuwa Mwanaume anapotaka kuvaa pambo kwanza azingatie unadhifu wa pambo la kiume uko vipi, pambo la kiume ni pete na unaweza kuvaa pete 1 mpaka 3 hata ukitaka kuvaa vidole vyote pia hukatazwi unavaa tu.
Sheikh Kundecha anasema, ukiachilia mbali mila na desturi za watu ambapo kufanya hivyo akitolea mfano wamasai na makabila mengine wao huvaa shanga kwenye sikio baada ya kulitoboa na kuvika shanga kama utamaduni wao na watu wameuzoea na si ajabu kumkuta akiwa hivyo na haishangazi.
Anasema, Uislamu hauna tatizo na mila na desturi ya mtu kama sio muislamu anaposilimu mmasai akawa muislamu basi mapambo ya kiume atalazimika kutoyafuata ikiwemo kutopamba sikio na kama alikuwa anavaa shanga ataacha kwasababu ni mila ya kimasai katika Uislamu mwanaume hapambi sikio maana hata kusuka nywele ni pambo la kike.
“Kwahivyo dhababu ni pambo la kike kwa chochote utakachokifanya sheria inasema isipokuwa dharura ya matumizi ya dhahabu na fedha katika maeneo ambayo yana maslahi kwa mfano mtu anaumwa kinywa na anapaswa kutumia kama tiba ataruhusiwa kwa manufaa hayo,” anafafanua Kundecha.
Aidha, Sheikh Kundecha anayataja madhara ya dhahabu kwa mawanaume kwa kusema, ”dhabau inaathari kimaumbile kwa mwanaume kama atavaa, inaweza kumlegeze mwili kumpotezea wasifu wa ukakamavu wa kimwili, maana sifa ya Mwanume ni kuwa mkakamavu.”
Anamalizia kwa kusema, “sifa ya kike ni kuwa mlegevu kwa mwanaume yeyote anayejilegeza anachukua wasifu wa kike na inapoteza maana ya yeye kuwa mwanaume na kwa mwanamke yeyote anayekuwa mkakamavu anachukua wasifu wakiume inamuondelea sifa ya yeye kuwa mwanamke na kufanya ukakamavu wa makusudi kufanana na mwanaume ni haramu.”