Bidahaa nyingi za vipodozi huongezwa mafuta ya nazi ndani yake, faida hasa ya mafuta hayo yanapaswa yawe ya asili, ambapo husaidia kudhibiti backeria, fugusi, sumu, vijidudu nyemelezi na maambukizi ya magonjwa.
Zifuatazo ni Faida za nazi katika mwili wa binadamu;
Hutibu tatizo la kupoteza kumbukumbu:
Tafiti nyingi zimeonyesha kuwa mafuta ya nazi yanao uwezo wa kuziamsha seli na shughuli za ubongo na katika kufanya hivyo kutasaidia kuzuia matatizo ya uwendawazimu au ukichaa (dementia) na kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).
Hutumika kulainisha uke mkavu:
Mafuta ya nazi yana matumizi mengi sana mwilini zaidi ya 100, kuna wanawake wana tatizo la kuwa na uke mkavu muda wote hata wakisisimuliwa vipi bado huwa wakavu, kuondokana na tatizo hilo pakaa mafuta ya nazi katika uke wako na utaona faida yake tena bila madhara yeyote hasi.
Husaidia katika ugonjwa wa mzio/aleji:
Moja ya faida ya mafuta ya nazi ni uwezo wa kudhibiti dalili za ugonjwa wa aleji, kila siku pakaa mafuta ya nazi ndani ya pua zako na uone kama utapiga chafya unapokuwa karibu na kile kinachokuletea aleji/mzio.
Huzuia maradhi mengi hatari mwilini:
Kama ilivyo katika kuipunguza kolesteroli, mafuta ya nazi yanao uwezo mkubwa katika kuzuia na kutibu magonjwa mengine sababu ya kuwa na kiasi kingi cha asidi iitwayo lauric acid.
Utafiti mwingi umeendelea kuthibitisha kuwa hii lauric asidi hubadilishwa kuwa asidi ijulikanayo kwa kitaalamu kama ‘monolaurin’ ambayo inayo sifa ya kudhibit na kuvizuia baadhi ya virusi ikiwemo vile vya ukimwi kuziingia na kuzidhuru seli za mwili na kusababisha maradhi mwilini.