Diamond Platinumz anazidi kupaa na kukubalika duniani na sasa sauti yake imeyakuna masikio ya familiaya wanamuziki nguli wa Marekani Swizz Beatz na Alicia Keys.

Kupitia Instagram, jana Swizz Beatz alipost video inayomuonesha mtoto wake akicheza wimbo wa Diamond ‘Nana’ pamoja na wimbo wa zamani ‘Nataka Kulewa’, walipokuwa kwenye gari. Hii ina maanisha kuwa nyimbo za Diamond ni moja kati ya nyimbo ambazo ziko kwenye orodha ya muziki wanaoukubali sana Swizz Beatz na familia yake.

Vibes ???? song by @diamondplatnumz #goodvibes

A video posted by therealswizzz (@therealswizzz) on

Diamond alitoa shukurani kwa familia ya Swizz Beatz kwa kusaidia kuisogeza Bongo Flava duniani.   

Mourinho Aukosoa Mfumo Wa Newcastle Utd
Magufuli: Sigombei Urais Kwa Majaribio, Nauweza