Dk. John Magufuli ambaye ni mgombea urais kupitia CCM, amewahakikishia wananchi kuwa amejipanga vilivyo kuishika nafasi ya urais kwa nia ya kuwatumikia wananchi na sio kufanya majaribio kwani anaiweza vilivyo.

Dk. Magufuli ametoa kauli hiyo alipokuwa akiwahutubia wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika Shinyanga ambapo aliwaomba wananchi hao kuhakikisha wanamchagua ili aweze kutimiza nia yake ya kuwatumikia wananchi wote na kuwaletea maendeleo wanayoyatarajia.

Dk. Magufuli aliwaahidi wananchi wa jimbo hilo kuwa akiingia ikulu atahakikisha kiwanda cha nyama kilichoko mkoani humo ambacho hivi sasa kinaonekana kupoteza muelekeo, kinafanya kazi ili kuongeza pato la wananchi wenye bidhaa ambazo zingeweza kutumiwa na kiwanda hicho.

Alituma ujumbe kwa mtu aliyebinafisishiwa kiwanda hicho kuhakikisha kinafanya kazi kabla hajaingia madarakani kwa kuwa endapo ataendelea kusuasua kufanya kazi atakirudisha serikalini.

“Wenyekiwanda wasikie, siku nikiapishwa kuwa rais wa Tanzania baada ya kuchaguliwa, wenye kiwanda hiki aidha kifanye kazi au wakirudishe serikalini Hatuwezi kukaa kwenye mkoa wa Shinyanga ambao una ng’ombe wengi halafu hakuna kiwanda cha nyama.”

Familia Ya Alicia Keys Yampa Shavu Diamond Platinumz
CCM: Ikulu Hapahitaji Mtunisha Misuli au Tyson