Mshambuliaji Wilfried Bony aliyerejea katika klabu ya Swansea City amesema familia yake ndio iliyomshawishi kwa kiasi kikubwa kurejea katika klabu hiyo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alikuwa akisakwa na vilabu mbali mbali barani Ulaya ikiwemo klabu ya Lille na Fenerbahce lakini amerejea katika klabu ya Swansea City aliyoihama mwaka 2015 na kujiunga na Manchester City.

“Nafikiri wanangu wawili wakiume wameamua hatma yangu,walisikia kwamba nilikuwa natakiwa na Swansea na wakaniambia ‘Baba lazima urudi Swansea’. Hivyo wanangu walichagua Swansea,” alisema Wilfried Bony.

Bony aliongeza kuwa hajutii kurejea Swansea kwani mashabiki wa klabu hiyo walimshangilia kila wakati aliporejea katika uwanja wa Liberty hata wakati akiwa Man City.

Kabla yakuondoka Swansea, Bony alicheza kwa kiwango kikubwa na kufanikiwa kufunga jumla ya mabao 34 lakini akiwa na Manchester City amefunga mabao 12 pekee.

 

 

Video: Jisalimisheni wenyewe kabla hatujaanza kuwakama- IGP Sirro
Mbowe aelezea maendeleo ya hali ya Tundu Lissu