Baada ya Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Fatma Karume kukosa nafasi ya kuhutubia katika siku ya sheria Februari 06, 2019, aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za binaadamu, Helen Kijo-Bisimba amesema kuwa anaamini kwamba waandaaji waliogopa kusikia vitu vingi vya siri alivyo navyo Fatma Karume.

Ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano na kituo cha redio kilichopo jijini Dar es salaam ambapo amesema kuwa sababu ya ufinyu wa muda iliyotolewa haina uzito mbele ya mdau wa sheria kama TLS.

“Mimi nakataa hakuna ufinyu wa muda kwa kuwa muda unapangwa. TLS ni mdau mkubwa wa mahakama. Kama ni ufinyu wangeondolewa watu wote na kuwaacha TLS. Kwa maoni yangu naona kabisa hawakutaka au walihofu kusikia kitu ambacho wao hawapendi kusikia”, amesema Kijo-Bisimba

Hata hivyo, siku moja kabla maadhimisho ya wiki ya Sheria, Rais wa Chama hicho, Fatma Karume alitoa taarifa kwamba,amepokea barua kutoka ofisi ya mwanasheria mkuu ya kumjulisha kuwa hatoweza kuhutubia umma kutokana na ufinyu wa muda.

 

Mahakama yasema sio kosa kuendesha ukiwa umekunywa pombe
Fatma Karume amuibua Bisimba, 'Wanamuogopa sana Fatma Karume'