Mabingwa wa Soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich huenda ikaipundua Manchester United kwenye dili la kuiwania huduma ya beki kisiki wa SSC Napoli, Kim Minjae katika dirisha la usajili wa majira ya Kiangazi, kufuatia ya mchezaji huyo kuonyesha uhitaji zaidi wa kutaka kuichezea Munich kuliko Man United.

Fundi huyu wa kimataifa wa Korea Kusini alidaiwa kufikia makubaliano binafsi na Man United lakini sasa mambo yanaonekana kubadilika na huenda akatimkia zake Ujerumani.

Kim ameshawishika zaidi na ofa ya Munich kwa sababu anaona huko ndio ataweza kushinda mataji tofauti na Man United ambapo timu ndio inajengwa kwa sasa.

Staa huyu amezivutia timu nyingi barani Ulaya kutokana na kiwango alichoonyesha msimu huu akiwa na Napoli ambayo ameisaidia kuchukua ubingwa wa Italia.

Inadaiwa ili kuipata huduma yake, Napoli inataka ofa isiyopungua Pauni 40 milioni. Kwa msimu uliopita fundi huyu amecheza mechi 45 za michuano yote. Mkataba wake unamalizika mwaka 2025.

AFCON 2024 kuivurugia Liverpool 2023/24
Sekretarieti ya Maadili ya viongozi yawapiga msasa wahariri wa vyombo vya habari