Uongozi wa klabu bingwa nchini Ujerumani, FC Bayern Munich, umemchimba mkwara meneja wa kikosi chao Pep Guardiola kwa kumwambia asitarajie kuondoka na mchezjai yoyote pindi safari yake ya kuelekea mjini Manchester itakapowadia mwishoni mwa msimu huu.

Meneja huyo kutoka nchini Hispania, amepigwa mkwara huo kutokana na baadhi ya vyombo vya habari kuanza kutoa taarifa za tetesi ambazo inadai kwamba kuna uwezekano mkubwa kwa Pep Guardiola akanufainika na hatua ya kuondoka na baadhi ya wachezaji huko Allianz Arena.

Gazeti la Daily Star la nchini England, limeripoti kwamba Pep Guardiola anajipa matumaini ya kuhama na mshambuliaji kutoka nchini Poland,

Robert Lewandowski kwa lengo la kwenda kuunda safu hatari ya ushambuliaji kwenye kikosi cha Man City ambayo kwa sasa inaongozwa na Sergio Aguero.

Abramovich Ajipanga Kuvunja Benki Kwa Ajili Ya Toni Kroos
Kampuni Ya Adidas Yafanywa Chambo Wa Kumnasa Paul Pogba