Nyota wa tenisi Roger Federer ameendeleza ushindi kwa asilimia mia katika mashindano ya wanaume ya tenisi ya dunia.
Federer alianza kwa kushinda seti ya kwanza kwa 7-5 kisha akapoteza seti ya pili kwa 4-6 kisha akamaliza kwa ushindi wa seti 6-4, dhidi ya Kei Nishikori wa Japan

Naye Novak Djokovic ambaye ni nyota namba moja kwa ubora aliendeleza wimbi la ushindi katika michuano hiyo kwa kumchapa Tomas Berdych.

Djockovic alipata ushindi wa seti mbili ambapo seti ya kwanza alishinda kwa 6-3 na kisha akamaliza kwa 7-5.

Djokovic atachuana na Rafael Nadal siku ya jumamosi huku Roger Federer akimsubiri mshindi wa Ijumaa kati ya Andy Murray au Stan Wawrinka.

Dirisha Dogo La Usajili Kufungwa Disemba 15
Wimbo Wa Taifa Wa Ufaransa Kusikika England