Hatimaye Kiungo kutoka visiwani Zanzibar Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ amefunguka hadharani kwa mara ya kwanza tangu alipoanza kushinikiza kuvunja mkataba wake na Klabu ya Young Africans mwishoni mwa  mwaka 2022.

Fei Toto amefunguka sakata lake na Young Africans alipofanya mahojiano na Clouds FM mapema leo Alhamis (Juni Mosi), ambapo ameseama amepitia kadhia nyingi hadi kufikai maamuzi ya kutaka kuvunjwa kwa mkataba wake.

Kiungo huyo ambaye alionekana kuwa msaada mkubwa katika kikosi cha Young Africans, hasa katika michezo ambayo ilikuwa mgimu kwa timu hiyo, amesema kwa muda wote alijitoa kuitumikia klabu, lakini manyanyaso yalikuwa machungu kwake na kujikuta akifanya maamuzi ya kujiweka pembeni.

Amesema Rais wa Young Africans Injinia Hersi Said amekuwa kikwazo kwake mara kadhaa, na mbaya zaidi amekuwa akisema uongo sambamba na kuwaaminisha Mashabiki na Wanachama wa klabu hiyo, anapoulizwa sakata linalohusu kuondoka kwake klabuni hapo.

Amesema kiongozi huyo alikuwa akimnyanyasa sana kwa kumtuhumu kuwa anauza mechi na kumwambia kuwa atarudi kwao Pemba, hali ambayo ilipelekea kumwaga machozi hadharani, na pia ikafika wakati injinia Hersi alikuwa hapokei simu yake.

“Injinia Hersi amenikejeli na ameniudhi sana, nimenyanyaswa sana nikiwa Yanga, nimeambiwa nauza mechi na viongozi.”

“Mara ya mwisho nimekutana na Hersi Mikocheni akaniambia anataka kunirudisha nikamwambia mimi siwezi, akaniambia basi nenda CAS.”

“Kama Rais sio Hersi sasa hivi narudi, sina shida na Yanga akiondoka Rais narudi sina shida na Mashabiki najua wananipenda.” Amesema Feisal

Katika hatua nyingine Feisal Salum akamzungumzia Mdhamini wa Young Africans Ghalib Said Mohamed, kwa kusema naye alimdharau kwa kushindwa kupokea simu zake wakati akitafuta suluhu ya tatizo lake, hivyo anaamini naye alimdharau.

“Pia Ghalib kaniudhi alikua hashiki simu zangu kabla, amenitafuta baada ya kuondoka na mimi sikupokea kwa sababu sipendi dharau hata kama sina kitu”

“Wakati natafuta suluhusho nilimtafuta Ghalib akawa hapokei baada ya kugoma akanitafuta sikumpokelea simu na, Mimi ni maskini lakini hata kama una pesa sitaki dharau”

Luciano Spalletti ajiweka pembeni SSC Napoli
Wizara itoe elimu matumizi sahihi ya Nishati - Waziri Mkuu