Baada ya kuiongoza SSC Napoli kutwaa Taji la kwanza la Serie A katika kipindi cha miaka 33, Meneja Luciano Spalletti anasema ataondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu na kuchukua muda wa mapumziko nje ya soka huku Luis Enrique akitajwa kuchukua mikoba yake.

Spaleti amesema anaona akili yake imechoka kufikiria na ndiyo maaana anahitaji kujipa muda wa kupumzisha akili yake kabla ya kufikiria tena kurejea kwenye mpira.

“Nahitaji kuchukua muda kupumzika kwa sababu nimechoka sana,” amesema na kuongeza

“Sijui kama unaweza kuiita sabato ya mwaka mmoja lakini sitafanya kazi. Sitakuwa nikifundisha SSC Napoli au timu nyingine yoyote.”

Spalletti mwenye umri wa miaka 64, ambaye alianza kukinoa kikosi cha SSC Napoli Julai 2021, alikuwa amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake.

Rais wa SSC Napoli, Aurelio De Laurentiis amesema ataheshimu uamuzi wa Meneja huyo.

“Yeye ni mtu huru, ametupa kitu na ninamshukuru, ni sawa kwamba anafanya anachotaka,” amesema Rais huyo.

Klabu hiyo imeshinda taji lao la kwanza Ligi Kuu ya Italia tangu Mei 4, 1990 ikiwa na michezo mitano mkononi huku pia ikifika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu 2022/23.

Meneja wa zamani wa AS Roma, Celta na FC Barcelona, Luis Enrique, ndiye anayetajwa kwa ukaribu zaidi kurithi kit cha Spaleti.

Nyuki wamvamia mtu aliyetaka kumtapeli mpenzi wake
Feisal Salum avunja ukimya Young Africans