Mashetani Wekundu (Manchester United) wapo tayari kumpa ruhusu ya kuondoka kiungo kutoka nchini Ubelgiji Marouane Fellaini pasina masharti ya malipo mwishoni mwa msimu huu, kuliko kumuweka sokini wakati wa dirisha dogo la usajili (Mwezi Januari 2018).
Mpango huo wa Man Utd kuwa tayari kufanya hivyo, umeibuka kufuatia mazungumzo ya kumsainisha mkataba mpya kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29 kutoonyesha matarajio ya kufikiwa kwa muafaka.
Mkataba wa Fellaini, unatarajia kumalizika Juni 30-2018, na umuhimu wake umeonekana kwenye kikosi cha Jose Mourinho na ndio maana viongozi wa Man Utd wanahaha ili kuhakikisha wanambakisha klabuni hapo.
Tayari Fellaini ameshakataa ofa ya kwanza ya kusaini mkataba mpya kwabuni hapo huku ikikataa bonasi ya Pauni milioni 4 ili kuhakikisha uhamisho wake unafaulu.
Fellaini alisajiliwa na Man Utd kwa dau la Pauni milioni 27, wakati wa utawala wa meneja David Moyes akitokea Everton inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini England.
Thamani yake kwa klabu ya United imeshuka, na pia hapendwi tena na mashabiki. Alizomewa na mashabiki wa klabu hiyo mwezi Disemba 2016 alipokuwa akipasha misuli yake moto kuingia uwanjani kama nguvu mpya walipokuwa wakikabiliana na Tottenham katika uwanja wa Old Trafford.
Alifunga bao katika nusu fainali ya ligi ya Uropa dhidi ya Celta Vigo na pia kuanza waliposhinda 2-0 dhidi ya Ajax kwenye fainali.
Mwanzoni mwa msimu huu Fellaini, alihusishwa na mipango ya kutaka kuhamia Galatasaray, lakini Meneja wa Man Utd Jose Mourinho alisema klabu hiyo ya Uturuki ilikuwa na nafasi nzuri sana ya kumsaini yeye mwenyewe kuliko Fellaini.
Inaaminika kwamba Fellaini amekuwa na uhusiano mwema na Mourinho, jambo ambalo huenda likawa muhimu katika kuamua mustakabali wa mchezaji huyo.