Klabu ya Galatasaray ya Uturuki inatarajia kutuma ofa ya kumsajili beki wa pembani kutoka England na klabu ya Arsenal Kieran James Ricardo Gibbs.

Gibbs amewekwa kwenye orodha ya wachezaji wanaaouzwa katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya kiangazi, na tayari klabu za Watford na Newcastle United zimejaribu kumsajili bila mafanikio.

Gibbs kwa sasa amesaliwa na mkataba wa mwaka mmoja, na hatosainishwa mkataba mwingine kufuatia kupatikana kwa mbadala wake Sead Kolasinac, aliesajiliwa akitokea Schalke 04 ya Ujerumani.

Vyombo vya habari nchini Uturuki vimeeleza kuwa, Galatasaray watatuma ofa ya Pauni milioni 4, kwa ajili ya kukamilisha dili la uhamisho wa beki huyo mwenye umri wa miaka 27.

Ali Kiba aliamsha dude, anamkejeli Diamond ‘Malkia wangu wa Nguvu...’
Kikwete: Wanaosubiri kustaafu ndipo waanze kilimo, ufugaji wamechelewa