Mpango wa meneja wa klabu ya Chelsea Antonio Conte wa kumuondoa kiungo kutoka nchini Hispania Cesc Fabregas katika kikosi chake umefahamika, ikiwa bado siku mbili kabla ya dirisha la usajili halijafungwa.

Gazeti la michezo la nchini Italia (Gazzetta dello Sport) limeripoti kuwa, Antonio Conte amedhamiria kumuuza Fabregas katika klabu ya Inter Milan kwa makubaliano maalum ya kubadilishana na kiungo wa klabu hiyo Marcelo Brozovic.

Conte anatajwa kupanga mpango huo, baada ya kuona kuna ugumu wa kumng’oa Brozovic huko Giuseppe Meazza katika kipindi hiki, kufuatia thamani ya ada yake ya usajili kuwa kubwa.

Meneja huyo anajiandaa kuwasilisha sehemu ya fedha ambazo hazikutajwa na gazeti hilo kwa kumjumuisha na Fabregas ili kukamilisha matakwa ya Chelsea ya kumpata kwa urahisi Brozovic.

Tayari uongozi wa klabu ya Inter Milan umeshagoma kumuuza Brozovic katika klabu za nchini Italia kwa kuhofia ushindani utakaowakabili katika michezo ya ligi ya Serie A, na badala yake wameonyesha kuwa tayari kumpeleka katika ligi yoyote.

Nape azifungia Magic FM na Radio 5 Kwa uchochezi
Shkodran Mustafi Afichua Siri Ya Kuwa Mshika Bunduki