Mgombea wa Urais kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ,John Magufuli ,ambae anasaka nafasi ya kuchangulia katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba mwaka huu. Amehaidi kujenga barabara ya kutoka Geita hadi kahama kwa kiwango cha lami.
Akihutubia wanachama wa CCM na wananchi wilani Chato mkoa Geita ,amesema kuwa atasimamia ilani ya chama hicho kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo itakayoboresha utalii katika eneo la kanda ya ziwa .
“Barabara ya Geita, Bukori hadi Kahama tutaijenga kwa lami mara tu mtakapomaliza kutuchagua. Na haya tumeyafafanua vizuri kwenye kitabu cha ilani ya uchaguzi ya CCM,” amesema Magufuli.
Magufuli amesema kuwa serikali ya CCM inajenga uwanja mkubwa wa ndege pamoja na daranja la Busisi mkoani Mwanza ili kuongeza na kukuza soko la utalii.
“Tunajenga uwanja mkubwa pale Mwanza, watalii wawe wanatoka Ulaya wanateremka Mwanza wakishatoka wasihangaike kupanda Kivuko na watapita kwenye daraja la Kilomita 3.2 pale Kigongo BusisI ambalo nalo ni utalii tosha”amesema Magufuli.
Bofya hapa …