Mamlata ya Mapato nchini TRA, imeitambulisha Kampuni ya Geita Gold Mining Ltd. (GGML), kwa mara nyingine kuwa mlipa kodi wa viwango vya juu katika sekta ya madini kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Tuzo hizo, zilipokelewa na Meneja Mwandamizi wa Fedha wa GGML, Ikingo Gombo na Meneja Utatuzi wa Migogoro ya Kodi wa GGML, Godvictor Lyimo kutoka kwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye.
Kmpuni hiyo, pia imetambuliwa kwa kuzingatia kiwango bora cha thamani ya bidhaa zilizosafirishwa nje ya nchi mwaka 2021/2022.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Hamad Chande alikabidhi tuzo hiyo kwa Meneja Mwandamizi wa Fedha kutoka GGML, Ikingo Gombo na Meneja Utatuzi wa Migogoro ya Kodi Godvictor Lyimo wa GGML.