Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Usalama Barabarani, UNRSF umezindua toleo la pili la kampeni yake ya kimataifa ya #moments2live4 ili kuifahamisha Duniani kuhusu athari mbaya za barabara zisizo salama kwa watoto na waathirika wa ajali za Barabarani.

Kwa mujibu wa UNRSF, mtu mmoja hufariki dunia barabarani kila baada ya sekunde 24 na kila baada ya saa 24 ambapo watoto 500 hufariki dunia kwa ajali barabarani pekee huku asilimia 93 ya vifo milioni 1.3 vya barabarani duniani na majeraha mabaya vikifikia milioni 50 na hutokea katika nchi za kipato cha chini na cha kati.

Mfuko huo kupitia taaarifa yake umeeleza kuwa, “Uhamasishaji ni hatua ya kwanza kuelekea kukabiliana na changamoto ya kimataifa ya usalama barabarani, maelfu ya mashirika na zaidi ya serikali 100 kwa sasa wako katika upande wa kutochukua hatua, na kwa kiasi kikubwa hawajui hatari kubwa kwa watumiaji wetu wa barabara walio hatarini zaidi ni watoto wetu.”

Askari akiwasaidia watoto kuvuka barabara nchini Afrika ya Kusini. Picha ya TimesLIVE.

Kampeni hiyo, inanuiwa kumwezesha kila mtu kupata ujuzi kuhusu jinsi ya kusaidia kuwaweka watoto salama barabarani, ambapo Mkuu wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Usalama Barabarani, Nneka Henry akisema, “kwa msaada kutoka kwa waungaji mkono mbalimbali tunatumai kampeni hii itaanzisha msaada wa ziada kwa mamlaka ya Mfuko na kufanya kazi katika nchi zinazoendelea.”

Kampeni ya kimataifa ya #moments2live4 inashirikisha watu mbalimbali kuanzia kwa madereva wa magari za mashindano, watumbuizaji, wanariadha wa kiwango cha kimataifa na viongozi wa dunia kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa baada ya kujifunza kuhusu athari za barabara zisizo salama na matumizi mabaya ya barabara kwa watoto.

Baadhi ya Waungaj mkono wa kampeni hiyo, wanajivunia mtandao wa pamoja wa hadi wafuasi milioni 50 wa mitandao ya kijamii, ambao utakuwa muhimu sana katika kukuza umuhimu wa suala hilo miongoni mwa mamilioni ya familia ambazo huenda hazikuwa na ufahamu wa kutosha.

Argentina chali Kombe la Dunia 2022
KMC FC kuwakosa watatu ikiwavaa Singida Big Stars