Beki wa kati mpya wa Young Africans, Gift Fred amesema kuwa licha ya kusugua Benchi bado anaamini akipata nafasi ya kucheza atajituma na kuisaidia timu hiyo kufanya vyema katika michuano mbalimbali msimu huu 2023/24.
Gift Fred ni ingizo jipya kwa Young Africans msimu huu akitokea Uganda katika klabu ya SC Villa, lakini tangu ajiunge na klabu klabuni hapo ameshindwa kuitumikia timu hiyo mara kwa mara na akijikuta katika nafasi yake wakicheza mabeki Bakari Mwamnyeto na Ibrahim Baka.
Akizungumza jijini Dar es salaam, beki huyo amesema kuwa, ndio kwanza ameingia ndani ya Young Africans hivyo bado hana presha ya kukaa benchi kwani anaamini kuna michuano mingi ambayo itamfanya acheze na akipata nafasi atajitahidi kupambana ili kufanya vyema.
“Mimi sina presha ya sasa ya kucheza kwa kuwa ndio kwanza msimu umeanza hivyo ambacho kipo kwa sasa ni kuhakikisha kuwa naendelea kujituma mazoezini, na pale ambapo nitapata nafasi ya kucheza ili nimuonyeshe mwalimu kuwa nipo tayari.
“Hivyo siwezi kusema kuwa najisikia vibaya kukaa benchi hapana, kuna michezo mingi ipo mbeleni na naamini kuwa siku mwalimu akinipa nafasi nitaitumia kuonyesha ubora na uwezo wangu ili siku nyingine anipe tena nafasi.
“Kuhusu ushindani wa namba ndani ya Young Africans ni mkubwa kwa kuwa kuna mabeki wazuri hapa na wanacheza vyema hivyo ni wazi mpaka kucheza lazima uwe bora zaidi,” amesema beki huyo