Chelsea wamefikia makubaliano yenye thamani ya pauni milioni 1.7 kumuuza Olivier Giroud kwenda AC Milan.

Mshambuliaji huyo kutoka Ufaransa mwenye umri wa miaka 36 tayari katua Italia na kufanyiwa vipimo kuwa mchezaji mpya wa Milan.

Klabu hiyo Serie A inatakiwa kulipa ada ya awali ya Pauni 860,000 (Euro Milioni Moja) pamoja na pauni nyingine 860,000 za nyongeza kulingana na idadi ya michezo kwa mchezaji huyo na kufuzu kwa klabu kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Giroud alisaini mkataba mpya wa mwaka mmoja baada ya Chelsea kutumia kifungu mwenye mkataba wa awali, yote ili kupata walau pesa kwani alikuwa mchezaji huru.

Arsenal ilimuuza Giroud kwenda Chelsea kwa pauni milioni 18 mnamo Januari 2018, miaka sita baada ya kumsajili kutoka kikosi kilichoshinda taji la Ligue 1, Montpellier kwa pauni milioni 10.8.

Mshambuliaji huyo amefunga mabao 39 na Assists 14 katika michezo 119 wakati akiwa Stamford Bridge, akishinda mataji matatu pamoja na taji la Ligi ya Mabingwa mwezi Mei mwaka huu, Europa League na FA Cup.

AC Milan tayari walikuwa wamemsajili beki Muingereza Fikayo Tomori, pia kutoka Chelsea msimu huu wa joto, kwani walitumia chaguo lao la pauni milioni 25 kumnunua beki huyo mchanga baada ya kumtumia kwa mkopo wa miezi sita, na pia bado wanavutiwa na Hakim Ziyech na Tiemoue Bakayoko wote kutoka Chelsea.

Miamba hiyo ya Italia ilimaliza ya pili kwenye Serie A msimu uliopita, na kurudi kushiriki Ligi ya Mabingwa kufuatia kutokuwepo kwa miaka saba.

Ninja atia neno fainali kombe la Shirikisho (ASFC).
Mugalu: Msimu ujao nitafanya makubwa zaidi