Januari 10, 2023 Askofu Msafiri Mbilu wa Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, aliongoza Ibada ya mazishi ya Mchungaji Sabina Lumwe, ambaye ni miongoni mwa Wachungaji watatu wanawake wa mwanzo wa kanisa hilo kupewa daraja hilo huku Mchungaji Sabina akiwa mwanamke wa kwanza kusomea theolojia mwishoni mwa miaka 70.
Mchungaji Sabina Lumwe ambaye ni mama wa mfanyakazi mwenzetu wa Dar 24, Festo Lumwe alizaliwa Julai 21, 1960 katika Kijiji cha Lutindi , Korogwe Mkoa wa Tanga, akiwa mtoto wa pili wa familia ya Baba Mwageni Mtunguja na Mama Julia Mtunguja.
Mwezi mmoja baadaye (Agosti 1960) alibatizwa na miaka 15 baadaye (1975), alipata Kipaimara Lutindi Parish na alisoma Shule ya Msingi Lutindi kisha alijiunga na Shule ya Sekondari ya Wasichana na Kibosho na kuhitimu mwaka 1979.
Mchungaji Sabina Lumwe alifariki Januari 8, 2022 kwa maradhi ya Shambulio la Moyo, ambapo DataVision na Dar24 Media wanatoa pole kwa mwana familia yetu (Festo Lumwe), Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, familia nzima ya Mchungaji Lumwe wa Lutindi na Lushoto Mjini.