Januari 10, 2023 Askofu Msafiri Mbilu wa Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, aliongoza Ibada ya mazishi ya Mchungaji Sabina Lumwe, ambaye ni miongoni mwa Wachungaji watatu wanawake wa mwanzo wa kanisa hilo kupewa daraja hilo huku Mchungaji Sabina akiwa mwanamke wa kwanza kusomea theolojia mwishoni mwa miaka 70.

Festo Lumwe (wa pili kutoka kulia), akiwa na majonzi mara baada ya kumpoteza mama.

Mchungaji Sabina Lumwe ambaye ni mama wa mfanyakazi mwenzetu wa Dar 24, Festo Lumwe alizaliwa Julai 21, 1960 katika Kijiji cha Lutindi , Korogwe Mkoa wa Tanga, akiwa mtoto wa pili wa familia ya Baba Mwageni Mtunguja na Mama Julia Mtunguja.

Askofu Msafiri Mbilu wa Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, aliyeongoza Ibada ya mazishi ya Mchungaji Sabina Lumwe.
Dauka Somba (kulia), akiwa na Augustino Mgoi katika viunga vya Kanisa la KKKT Lushoto kushiriki Ibada ya mazishi.

Mwezi mmoja baadaye (Agosti 1960) alibatizwa na miaka 15 baadaye (1975), alipata Kipaimara Lutindi Parish na alisoma Shule ya Msingi Lutindi kisha alijiunga na Shule ya Sekondari ya Wasichana na Kibosho na kuhitimu mwaka 1979.

Afisa Mradi wa DataVision International, Macmillan George akiwa na baadhi ya waombolezaji kushiriki mazishi ya Mchungaji Sabina Lumwe nyumbani kwa Marehemu mjini Lushoto.
Ibada ya kumuombea Mchungaji Sabina Lumwe ikiendelea, enzi za uhai wake pia aliandika kitabu cha “My Marriage Are Not Start Yet.”

Mchungaji Sabina Lumwe alifariki Januari 8, 2022 kwa maradhi ya Shambulio la Moyo, ambapo DataVision na Dar24 Media wanatoa pole kwa mwana familia yetu (Festo Lumwe), Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, familia nzima ya Mchungaji Lumwe wa Lutindi na Lushoto Mjini.

Waombolezaji wakiingia Kanisani kwa ajili ya kuanza kwa Ibada.
Viongozi mbalimbali wa KKT wakiwasili Kanisani.
Waombolezaji wakiwa wamebeba shada za maua huku wakiingia kanisani kwa kuongozwa na wapigaji wa Tarumbeta

Morani wadaiwa kuwashambulia Viongozi CCM
Dkt. Mpango azitaka Halmashauri kufikia lengo upandaji miti