Chama cha Alliance For Democratic Change (ADC) kupitia mwenyekiti wake, Hamad Seif Mohamed na Msajili wa Vyama vya siasa, Francis  Mutungi wamemtaka Maalim Seif akubali kukaa na Mwenyekiti wake, Profesa Lipumba ili kutatua mgogoro uliopo baina yao.

ADC kimelaani vitendo vinavyofanywa na Maalim Seif vya kuwafukuza wanachama wenzake wakiwemo waasisi wa chama hicho, Mussa Haji Kombo na Nassor Seif Amour.

Hivyo Hamad amemshauri Maalim Seif kufanya mojawapo kati ya mambo matatu, akubali kukaa chini na mwenyekiti wake, aheshimu ushauri wa msajili wa vyama vya siasa Mutungi au ajiondoe kwa heshima katika uwanja wa siasa na kuwaachia wengine”.

Amesema akidai ubishi au kutaka kupimana misuli na msajaili wa vyama vya siasa ili kutaka maamuzi yake yawe sahihi kuliko matakwa ya katiba au kufukuza wenzake kila siku, hatutamsaidia kwa kuwa ameshawafukuza wengi na hajaambulia lolote.

Aidha amemalizia  na kusema” Kibri kwetu waumini wa kiislamu ni nguo ya Mungu, sifa ya kibri sio nzuri kulinganishwa nayo binadamu. Binadamu mzuri hukubali majadiliano mazungumzo na maafikiano. Ukaidi na ubishi ni nyenzo za kubomoa, sio kujenga jambo likawa”.

Amemaliza kwa kusema yanayotokea CUF ni mataokeo ya ubishi na kutoambilika kwa Maalim Seif.

Diamond kung'arisha upya nyota ya Mr. Nice
LIVE: Rais Magufuli akihutubia wananchi Handeni, Tanga