Mnamo mwaka 1808, gari la kwanza duniani liligunduliwa ambapo injini yake ilitengenezwa kwa mchanganyiko wa hidrojeni na oksijeni.
Aliyegundua gari hilo alijulikana kwa jina la Isaac De Rivaz raia wa Ufaransa na Uswiz, hata hivyo aina hiyo ya gari alilogundua haikufaulu katika matumizi yake, Pia wagunduzi wa Kimarekani, Samuel brown na Samuel Murray walishindwa kufaulu vizuri kama mgunduzi wa kwanza.
Baada ya miaka 24, Entiene Noire alifanikiwa kutengeneza injini lakini baada ya kuiweka kwenye gari ilikuwa ikifanya kazi taratibu kuliko hata binadamu. Mnamo mwaka 1886 Januari 26, Mgunduzi wa Kijerumani aligundua gari aina ya Karl Benz yenye ‘gasoline auto motor’ huko Ujerumani, na Karl Benz ndiye aliyekuwa wa kwanza kuanzisha msingi wa viwanda vya magari ya aoutomatic duniani, alitengeneza gari yenye matairi matatu kama gari ya kihistoria jijini kwake ‘roam’.
Baada ya hapo Gottlieb Daimler aligundua gesi na kutengeneza gari lake kwa kutumia hiyo gesi. Mwaka huo huo Machi, aina hiyo ya gari kwa mara ya kwanza ilitengenezwa yenye matairi manne, yenye enjini inayotumia mafuta mengi na ilikuwa tayari kutangazwa.
1889 Daimler alitambulisha injini mpya na baada ya mwaka mmoja Daimler aliitangaza rasmi Daimler kama kampuni yake mpya ya uzalishaji magari aina ya Daimler huko Ujerumani katika mji wa Stuttgart ili kuanza ushindani na makampuni mengine ya uzalishaji magari.