Ilivyoonekana Ofisi ya Tanganyika African National Union (TANU) mtaa wa Jaribu Magomeni Mapipa katika miaka ya 1950 na wanachama wake wakiwa wamezunguka Ofisi ya chama hicho.
TANU kilikuwa chama kilichotawala Tanganyika na Tanzania hadi muungano na Chama cha Afro-Shiraz cha Zanzibar ulipounda Chama cha Mapinduzi (CCM) mwaka 1977.
TANU ilianzishwa 7 Julai, 1954 kutokana na Tanganyika Afrikan Association(TAA). Mwenyekiti wa kwanza wa TANU alikuwa Julius Kambarage Nyerere na chama hicho kilishinda kila uchaguzi chini ya utawala wa kikoloni kikaongoza Tanganyika hadi ilipopata uhuru wake mwaka 1961.