Wakati wa urais wa Ali Hassan Mwinyi, sera za Ujamaa zilianza kugeuzwa. Badala yake sera za soko huru zilianzishwa, masharti ya kuingiza bidhaa kutoka nchi za nje yalipunguzwa na uanzishaji wa biashara ya watu binafsi ulihamasishwa. Mwaka wa 1991, uanzishaji wa vyama vingi uliruhusiwa.
Sera za soko huru za Mwinyi zimeendelezwa chini ya Rais Benjamin Mkapa. Mara baada ya kustaafu, Mwinyi hakujiingiza katika mambo ya siasa tena.
Mwinyi alikuwa Rais wa pili wa Tanzania kuanzia 5 November 1985 hadi 23 November 1995, kabla hajachaguliwa kuwa Rais, alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Makamu Rais. Pia alikuwa mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuanzia 1990 hadi 1996.
Amezaliwa 8 Mei 1925, Kisiwa cha Unguja Zanzibar.