Amtambulisha rasmi mrembo @briana__tz kuwa ndiye mpenzi wake mpya. Ni kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram ambapo ameweka picha kadhaa za mrembo huyo kutoka nchini Italy.

Harmonize amemtambulisha mrembo huyo kwa kuandika, ” nilikuwa nikiusubiri wakati huu kwa muda mrefu sana ili niuthibitishe umma ni kiasi gani una maana kubwa kwenye maisha yangu”

Kitendo hicho kimeambatana na maamuzi ya msanii huyo kuwa-unfollow watu wote aliokuwa amewafuta kupitia mtando wa Instagram na kumbakiza mpenzi wake pekee.

Novemba 15, 2021. Harmonize aliwaomba radhi kwa kuwa-unfollow watu wote aliokuwa amewa-follow kwenye mtandao huo kwa kusema “nawapenda wote lakini nataka kumfuata mpenzi wa maisha yangu, hivyo msijisikie vibaya baada ya kuwa-unfollow, ninawapenda na kuwaheshimu sana”.

Mlipuko wa 3 wapangwa Kampala
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Novemba 17, 2021