Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane amefunga mabao mawili katika mchezo ambao timu ya taifa ya Uingereza imeibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya timu ya taifa ya Malta.

Kane ambaye alikuwa na ukame wa mabao baada ya kutofunga bao lolote mwezi Agosti aliipatia Uingereza bao la kuongoza mnamo dakika ya 53 baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Dele Alli kabla ya Ryan Bertrand kuongeza bao la pili dakika ya 86.

Katika mchezo huo wa kuwania kushiriki katika michuano ya kombe la dunia mwaka 2018 timu ya Uingereza ilifanikiwa kufunga mabao yake katika dakika za mwisho za mchezo huo baada ya Danny Welbeck kufunga bao la tatu dakika ya 91 na badae Harry Kane kuongeza bao la nne sekunde kadhaa kabla ya mchezo huo kumalizika.

Baada ya ushindi huo kikosi cha Uingereza kinachonolewa na kocha Gareth Southgate kinaongoza kundi ‘F’ lenye timu za Malta,Slovakia,Scotland,Slovenia na Lithuania kwa pointi 17 baada ya kucheza michezo 7.

Harry Kane akifunga bao la kwanza

Timu ya Slovakia inashika nafasi ya pili katika kundi hilo ikiwa na pointi 15 baada ya kucheza michezo saba huku Malta ikiburuza mkia katika nafasi ya sita ikiwa haina pointi baada ya kucheza michezo saba.

 

Mimba za utotoni zakithiri mashuleni
Video: Kichupa kipya Patoranking Ft Diamond Platinumz 'Love you Die'