Kocha Mkuu wa JKT Tanzania, Malale Hamsini amesema anaendelea kumtengeneza nyota wake, Hasan Dilunga ili kurejea kwenye ubora wake, akitamba kuwa baada ya misimu miwili huenda asibaki kikosini humo.

Dilunga aliyewahi kuzichezea timu kadhaa, mara ya mwisho alikuwa akiitumikia Simba SC kabla ya kupata majeraha ya kifundo cha mguu ‘Enka’ iliyomuweka nje kwa zaidi ya msimu mzima.

Kwa sasa kiungo huyo mshambuliaji anakipiga JKT Tanzania ikiwa ni mipango yake kusaka nafasi ya kucheza ili kujiimarisha zaidi na kurejea rasmi uwanjani na sasa ameanza kutoa matumaini.

Kocha Hamsini amesema licha ya kwamba nyota huyo bado anajitafuta, misimu miwili ikiisha atakuwa mpya na huenda asibaki kikosini humo akisema kuwa anampangilia vyema ratiba za mechi kwamba hali yake inaimarika.

“Niliwahi kuwa naye nyuma kabla ya sasa hivyo namuona mwanangu mbali na kufanya naye kazi kimaisha, naendelea kumfua na ninaamini atawashangaza wengi na ndani ya misimu miwili sidhani kama atabaki hapa,”

Kwa upande wake Dilunga alisema: “Nimetoka kwenye majeraha ya muda mrefu, hivyo ninachofanya ni kutumia dakika chache ninazopata kujiweka sawa.

Declan Rice apongeza upambanaji Arsenal
Vita ya Alphonso Davies yapamba moto Ulaya