Mkurugenzi wa uwekezaji wa kampuni ya GSM ambao wamejipanga kufanya Usajili mkubwa ndani ya klabu hiyo, Mhandisi Hersi Said amesema hawana mpango wa kumsajili mchezaji yoyote kutoka Simba SC.

Hersi ametoa msisitizo huo, kufuatia mipango ya klabu ya Young Africans kuendelea kuhusishwa na taarifa za kuwanyemelea baadhi ya wachezaji wa mabingwa hao wa Tanzania bara, huku jina la kiungo Said Ndelma likiongoza kwenye orodha ya wachezaji wanaohusishwa kutua Jangwani.

Ndemla amekuwa akihusishwa na tetesi za usajili ndani ya klabu ya Young Africans, uvumi ambao umekuwa ukijitokeza kila msimu wa dirisha la usajili, unapowadia.

Amesema wanaheshimu ubora wa wachezaji wa Simba pamoja na Ndemla lakini katika orodha wanayoifanyia kazi hawana jina lolote kutoka kwenye klabu ya Simba, kwani wanataka kusuka kikosi cha aina yake na chenye ubora mzuri na wakipekee zaidi ya klabu zote nchini Tanzania.

“Ndemla Aje wapi Yanga, Hapana huo uvumi tu! ni mchezaji mzuri mwenye uwezo mkubwa, lakini mpaka sasa hatuna jina lolote la mchezaji kutoka Simba, Yanga tuna hesabu tofauti za usajili. Tunataka vitu vikubwa safari hii.”

“Huku tutaleta watu wa kweli wanaokuja kuanza kikosi cha kwanza kwa sababu huko wanakotoka tumeridhika na ubora wao, hatuleti watu wa kujaribu, huo ndio mpango wetu kwa sasa Tunachotaka kufanya kuna watu ambao tuta achana nao hasa wale ambao wamekuwa wakikosa nafasi.”

Kampuni ya GSM ambayo ni sehemu ya wadhamini wa klabu ya Young Africans, imekua mstari wa mbele katika kufanikisha klabu hiyo inafanya usajili mzuri, baada ya kufanya hivyo wakati wa dirisha dogo la usajili na kufanikisha ushindi dhidi ya Simba Machi 08.

Walevi wageukia 'Soseji moja na bia mbili' kukabili zuio la kufungwa bar
Simba SC wakumbuka 2012