Baada ya tetesi na mvutano wa muda mrefu kati ya Chelsea na Diego Costa hatimaye mshambuliaji huyo anahamia Athletico Madrid baada ya klabu hiyo kukubaliana na Chelsea.
Taarifa zinasema ndani ya masaa 24 kuanzia sasa mshambuliaji huyo anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya na anaweza kutangazwa kama mchezaji wa klabu hiyo ndani ya muda mfupi.
Costa aligoma kabisa kurudi katika klabu ya Chelsea licha ya klabu hiyo kuliweka jina lake katika majina ya wachezaji watakaoitumikia katika Premier League.
Tangu mwanzo mshambuliaji huyo alionyesha matamanio yake kurudi Athletico Madrid kwa kuweka wazi kwamba asingependa kubaki Chelsea kwani hakuwa na mahusiano mazuri na kocha Antonio Conte.
-
Everton yamkata Rooney mshahara wa wiki mbili
-
Video: Real Madrid yaangukia pua, yapigwa na Real Betis
-
Karim Mostafa Benzema hadi 2021
Pamoja na makubaliano baina ya Athletico Madrid na Chelsea juu mchezaji huyo hawataweza kumtumia kwa sasa kwani wanatumikia kifungo cha usajili hivyo itamlazimu Costa kusubiri hadi January kuvaa jezi ya Athletico Madrid kwa mara nyingine.
Chelsea walimsajili Diego Costa kutoka Athletico Madrid mwaka 2014 kwa ada ya Pauni milioni 32 na sasa wanamuuza kwa ada ya Pauni milioni 53 kurudi tena katika klabu yake hiyo ya zamani.
Diego Costa tangu ajiunge Chelsea amewafungia jumla ya mabao 52 katika michezo 89 huku akichangia kutoa ‘assist’ 16 na msimu uliopita aliwasaidia kubeba kombe la Premier League.