Waziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Leo Julai 1, 2021 amefanya ziara ya siku moja nchini Burundi yenye lengo la kuimarisha uhusiano wa Tanzania na Burundi
Akizungumza na Dar24 Media katika kipindi cha mahojiano na mchambuzi wa siasa Said Miraj amesema kuwa umuhimu wa ziara kwa viongozi wa nchi kufanya katika nchi jirani ni faida kwa maendeleo ya nchi kwenye sekta mbalimbali.
Amesema kiongozi anaposafiri anaenda kama taasisis inayoambatana na baadhi ya wadau waserikali na wasio wa kiserikali kama vile wafanyabiashara ambapo hii inasaidia kupanua wigo wa maendeleo na kuwapata fursa walio walienda na kiongozi katika mikutano itakayokuwa inafanyika na kubadilisha mawazo katika kukuza maendeleo baina yao.
Halikadhalika Mchambuzi Said Miraj ameongeza kuwa ziara inasaidia kukuza mahusiano ya kimataifa baina nchi, ambapo mahusiano ya kimataifa ni mwelekeo wa maendeleo ya fursa za kibiashara.