Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Tanzania Bara Simba SC Didier Gomes, amesema ameangalia kwa makini michezo minane ya Young Africans hivyo anajua jinsi ya kuwakabili.

Gomes amesema katika mchezo wa mzunguko wa kwanza aliona mapungufu ya Simba SC na wao kama benchi la ufundi wamejitahidi kuyafanyia kazi.

Amesema kuna wachezaji Young Africans wana uwezo mkubwa lakini Simba haitaingia kwa kuangalia mchezaji mmoja mmoja badala yake tumejipanga kuikabili timu nzima.

“Nimetazama michezo yao minane ya hivi karibuni hivyo kuna vitu tumeviona ambavyo tunaamini vitatusaidia kupata ushindi, tunajua mchezo utakuwa mgumu lakini tupo tayari
kupambana,” amesema Gomes.

Gomes amekiri licha ya ugumu uliopo kwenye mchezo huo lakini lengo ni moja tu kuhakikisha tunapata ushindi ili hatimaye tuchukue ubingwa kwa mara ya nne mfululizo.

Simba SC inaongoza msimamo wa Ligi Kuu kwa kuwa na alama 73, ikifuatiwa na Young Africans yenye alama 67, huku Azam FC wakishika nafasi ya tatu kwa kuwa na alama 64.

Ally Saleh atimiza ahadi yake
Hii ndiyo siri ya ziara kwa Viongozi