Mwanafunzi mmoja nchini Nigeria aliyehitimu mafunzo ya sheria mwenye dini ya Kiislamu amezuiwa kufuzu elimu hiyo baada ya kwenda kinyume na uvaaji wa vazi rasmi lililowekwa na vyuo vya sheria kuvaliwa siku ya kuhitimu mafunzo hayo.
Mwanafunzi huyo anayejulikana kwa jina la Amasa Firdaus, ambaye amefuzu kutoka chuo cha Ilorin, alizuiwa kuingia katika ukumbi wa kufuzu kwenye mji mkuu Abuja ambapo sherehe zilikuwa zikifanyika.
Ambapo alikataa kuvua Hijab yake kutokana na sababu za kidini zinazomzuia mwanamke kuonesha kichwa chake.
Kupitia taratibu hizo za kidini mwanafunzi huyo aligoma kuvua Hijab na kuomba huku akisisitiza kuvaa kofia hiyo ya kufuzu juu ya Hijab yake.
Hii ilitajwa kuwa ni kwenda kinyume na vazi ramsi lililoweka na vyuo vya sheria.
Hata hivyo mtumiaji mmoja wa mtandao wa Instagram alisema kuwa Bi Firdaus ana haki ya kufanya hivyo.