Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla leo Novemba 19, 2021 ametembelea ujenzi wa kiwanda kikubwa na cha kisasa cha uzalishaji wa nyaya za umeme za majumbani na nje pamoja na Transformer cha ELSEWEDY ELECTRIC ambapo amesema ujenzi wa kiwanda hicho umekuja wakati muafaka ambapo Serikali ipo kwenye kasi ya usambazaji wa umeme Vijinjini.
RC Makalla amesema mbali na kiwanda kusaidia upatikanaji wa nyaya na Transformer pia kinakwenda kutoa ajira kwa zaidi ya vijana 500 wa kitanzania hivyo kusaidia kutatua tatizo la ajira.
Aidha RC Makalla amesema uanzishwaji wa kiwanda hicho na viwanda vingine vilivyopo itasaidia kuweka ushindani wa kibiashara na kuleta unafuu wa bei kwa wateja na kukuza Soko la Africa Mashariki.
Hata hivyo RC Makalla amewapongeza wawekezaji wa kiwanda hicho cha Elsewedy Electric kwa kuichagua Tanzania Kama sehemu salama kwa uwekezaji na kueleza kuwa serikali itaendelea kutoa ushirikiano na kuweka mazingira Bora ya kibiashara.
Kwa upande wake Afisa Rasilimali watu wa kiwanda hicho Gabriel Mpongole na Mhandisi wa Viwango Delain Mwakalasi wamshukuru RC Makalla kwa kuwatembelea na kueleza kuwa lengo la badae ni kuanzisha pia kiwanda cha uzalishaji wa maungio ya nyaya za umeme, mita za umeme, maji na chuo cha ufundi cha kuzalisha wataalamu wengi zaidi.