Mbunge wa Viti Maalum Nusrat Hanje, ameibua hoja ya wahitimu wa darasa la saba waliopitia vyuo vya ufundi kutokupewa nafasi za kazi derikalini licha ya ufanisi walio nao baadhi yao.
Akizungumza Bungeni leo Mei 27, 2021 Hanje amehoji “Ni kwanini vijana waliomaliza darasa la saba hawapewi fursa ya kuajiriwa na taasisi za serikali hata kama wanazo fani walizozipata kupitia vyuo vya ufundi VETA vinavyotambulika na serikali kwa kigezo cha kutokuwa na cheti cha kidato cha nne?”
IGP Sirro awanyoshea kidole Kinondoni, “vinara wa uhalifu”
Akijibu swali hilo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema, ”Ni kweli upungufu ugumu wa upatikanaji wa ajira na changamoto ya ajira ipo duniani kote ikiwemo Tanzania, lakini kila serikali inaweka utaratibu mzuri kushughulikia changamoto hii, serikali inao mkakati wa kuanzisha viwanda vitakavyoweza kutoa ajira kwa watu wote.”
Hanje ameiomba serikali iangalie namna ya kuwaajiri wanaohitimu VETA kwani vyuo hivyo vinatambulika.