Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan aliyoitoa Septemba 23 kwenye Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) New York nchini Marekani, imetajwa kuwa miongoni mwa hotuba saba muhimu zaidi kwenye kikao hicho.

Aidha hotuba imechaguliwa na tovuti ya Marekani ‘Foreign Policy (FP)’ miongoni mwa hotuba muhimu zaidi kutolewa kwenye kikao hicho na pia ni ya pekee kutoka kwa mkuu wa nchi mwanamke.

Rais Samia amekuwa mmoja wa wakuu wachache wa nchi wanawake kutoka Afrika kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Viongozi wengine ambao hotuba zao zimeelezea mambo muhimu ni pamoja na Rais wa China Xi Jinping, Rais wa Marekani Joe Biden, Rais wa Brazil Jair Bolsonaro, Rais wa Lebanon Michel Aoun, Rais wa Iran Ebrahim Raisi na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi.

Katika chapisho lao ‘FP’ liliwataka wachangiaji na waandishi wa kurasa zao kupima hotuba wanazoona zina uzito mkubwa au zina mambo muhimu zaidi.

Makubaliano ya Doha chanzo cha Afghanistan kuwa mikononi mwa Taliban
Serikali kuja na mikakati ya ulipaji kodi na misamaha