Mbunge wa jimbo la Mtama kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amesema kuwa kuchanganya shughuli za kijeshi na masuala ya kisiasa inaleta ukakasi.
Amesema kuwa kuna wakati inakuwa ni vigumu sana kumtofautisha Rais wa nchi na Mwenyekiti wa CCM kwa kuwa mtu huyo anakuwa ni mmoja na kwenda mbali zaidi kuwa kuna wakati huwa kuna kuwa na mvutano kati ya wanachama na viongozi wa ulinzi na usalama katika baadhi ya matukio ambayo Rais anahudhuria.
“Bahati mbaya ni ngumu sana kumtofatisha Magufuli Rais wa Tanzania na Magufuli Mwenyekiti wa CCM kwa kuwa huyu mtu ni mmoja kwamba yeye ndiye mwenye vyeo vyote viwili lakini ni rahisi kuzitofautisha shughuli kwamba anapofanya mambo ambayo yanaihusu taasisi ya Urais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kusichanganywe na shughuli za CCM inawezekana ikafanyika hivyo.”amesema Nape