Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imerejesha huduma ya ibada katika makanisa baada ya takribani miezi mitano iliyopita tangu kfungwa kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.
Jumapili ya Agosti 16, 2020 mamia ya wakristo nchini humo wamejumuika kwa pamoja katika sala wakiwa na shangwe kubwa huku makanisa yakiwa na vifaa vya kunawia mikono na vipima joto ambapo kila mkristo alitakiwa kuvaa barakoa.
Pia, ibada hizo zimewagawa waumini kuingia kwa awamu katika ibada ili kupunguza msongamano ambapo hatua hii imekuja wakati ambao baadhi ya waangalizi wakihofia kuongezeka zaidi kwa visa vya maambukizi ya corona.
Hata hivyo kwa sasa DRC, imefungua mipaka yake na usafiri wa ndege na gari unaruhusiwa kutoka jimbo moja kwenda jimbo lingine.