Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Ibrahim Class amefichua kuwa amepanga kumfundisha ngumi mpinzani wake Said Chino kuelekea katika pambano la Usiku wa Classic linalotarajia kupigwa Mei 27, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Warehouse Masaki.

Class ametoa kauli hiyo kufuatia mpinzani wake, Said Chino kuanza kugomea pambano hilo kuchezeshwa na mwamuzi Pendo Njau kwa madai ya kuwa na ukaribu na mpinzani wake.

Class amesema kuwa anashukuru Mungu kuwa amejiandaa vizuri kuelekea katika pambano hilo huku akiahidi mashabiki wake ushindi wa KO.

“Nashukuru Mungu nimejiandaa vizuri kuelekea katika pambano langu na Said Chino kwa sababu nafanya mazoezi ili nishinde na hata yeye anafanya mazoezi ili aweze kushinda lakini mimi nina uhakika nawaambia mashabiki zangu ushindi upo paleple na sina kazi mbovu.”

“Watanzania kama wanavyonijua, nitaonyesha kazi nzuri na kila mtu atafurahia mchezo wangu na nitamfundisha Said Chino ngumi zinapigwa vipi na siyo maneno yakuongea haipo hivyo, tunafanya kazi maneno baadae kwa sababu Chino ni bondia wa kawaida sana ambaye ana maneno mengi halafu vitendo hakuna na watu kama hao dawa zao ninazo.” amesema Class

Thierry Manzi afunguka kutua Simba SC
Polisi yafafanua tukio aliyekufa kwa kujirusha toka Ghorofani