Idadi ya watu walionyongwa duniani kote imeongezeka kufikia asilimia 53 mwaka 2022 zaidi ya mwaka uliopita, kukiwa na ongezeko kubwa nchini Iran na Saudi Arabia.
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesema katika ripoti ya kila mwaka ambayo pia ilikosoa Indonesia kwa idadi kubwa zaidi ya hukumu za kifo barani Asia.
Amnesty imesema, asilimia 70 ya watu walinyongwa Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, na ilitekelezwa zaidi Iran, ambapo idadi yao imeongezeka kwa asilimia 83 kutoka 314 mwaka 2021 hadi 576 mwaka 2022.
Idadi ya walionyongwa nchini Saudi Arabia imeongezeka mara tatu kutoka 65 mwaka 2021 hadi 196 mwaka 2022 ambapo ongezeko hilo pia limerekodiwa nchi za Kuwait, Myanmar, Palestina, Singapore na Amerika.