Mapema hivi karibuni, Mchungaji Eliud Wekesa, maarufu kama Yesu wa Tongaren raia wa Magharibi mwa Taifa la Kenya, alijisalimisha Polisi kwa mahojiano baada ya kutakiwa kufanya hivyo ikiwa ni hatua mojawapo ya Serikali ya nchi hiyo kuwadhibiti wahubiri wenye misimamo na itikadi kali.

Siku moja baadaye, akapandishwa Mahakamani mjini Bungoma kwa tuhuma za kutiliwa shaka kwa mafundisho yake ya kidini, huku yeye akijitetea kuwa hana hatia na kwamba anafanya kazi ya kueneza injili kwa viumbe waliopotea.

Baadaye akawekwa kizuizini kwa siku nne zaidi, ili kutoa nafasi kwa uchunguzi dhidi yake wakati vyombo vya usalama vikifuatilia uchunguzi dhidi ya mafunzo yake yanayodaiwa kuwa ni potofu yanayotolewa katika kanisa lake.

Mara baada ya muda huo wa kukaa ndani kuisha hatimaye akapandishwa tena kizimbani kwa hukumu, na sasa mbele ya Mahakama ya Bungoma, Hakimu mkuu, Tom Olando amemwachilia huru bila vikwazo akisema wapelezi wa ofisi ya DCI wamekosa ushahidi dhidi yake na kwamba mtuhumiwa hana kesi ya kujibu.

Tukio hili linajiri huku Mchungaji mwingine Ezekiel Odero wa Kanisa la New Life Prayer Centre and Church lililopo Kaunti ya Kilifi, akiwasilisha ombi lingine mahakamani la kutaka akaunti zake za benki zifunguliwe baada ya kuwa nje kwa dhamana.

Pastor Odero anakabiliwa na kesi ya kuhusishwa na uhubiri wa imani kazi na ushiriki wa mauaji ya watu zaidi ya 200 waliokufa kwenye shamba la mchungaji mwingine, Paul Mackenzie aliyewaambia waumini wake wafunge kula na kunywa ili wafe wapate nafasi ya kwenda kukutana na MUNGU wao.

Mfumania nyavu Afrika Kusini awaniwa Jangwani
Robertinho, Nabi watajwa Taifa Stars