Kocha Msaidizi wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, Hemed Morocco amesema makocha wa Simba SC na Young Africans wana msaada mkubwa kwenye timu hiyo kwani wanawapa wachezaji wazawa nafasi ya kucheza.

Morocco amesema makocha wanaofundisha Ligi Kuu wana mchango mkubwa kwa timu hiyo lakini kutokana na Simba SC na Young Africans kutawaliwa na wachezaji wa kigeni kuliwanyima nafasi kubwa wazawa kupata namba.

Kocha huyo amesema kuna umuhimu kwa makocha wa Ligi Kuu kuwa na ubunifu wa kuwatumia wachezaji wazawa ili kuendeleza viwango vyao.

“Makocha wote wana msaada mkubwa kwetu sisi Stars kutokana na kuwa na wachezaji wengi wa kigeni jambo linalowapa tabu wazawa kupata nafasi, lakini sio kwamba Tanzania hatuna vipaji tunavyo ila namba ndio tatizo,” amesema Morocco

Amesema kitendo cha kocha wa Simba SC, Robert Oliveira ‘Robertinho’ kumtumia Kibu Denis wakati ambao watu hawamhitaji kunasaidia kuinua uwezo wake na taifa kwa jumla.

Pia ametolea mfano Kocha wa Young Africans, Nasreddine Nabi kuamini uwezo wa Clement Mzize na kumpa nafasi ya kucheza hadi mechi za kimataifa kunamwongezea mchezaji kujiamini na kufanya vizuri.

Mahakama yataja sababu kumuachia huru Yesu
Roul Shungu akoleza moto Afrika Kusini