Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amesema kuwa anawasiwasi kuwa uamuzi wa kuruhusu idadi kubwa ya mashabiki kuhudhuria mechi za michuano ya kandanda barani Ulaya ya Euro 2020 utaongeza kiwango cha maambukizi ya virusi vya corona.
Amesema hayo akiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari pamoja na Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson, Merkel amesema ana mashaka juu ya iwapo uamuzi huo ulikuwa wa busara katika kipindi ambapo kirusi cha corona aina ya Delta kimezidisha idadi ya maambukizi barani Ulaya.
Aidha amesisitiza kuwa hana mpango wa kuamuru kupunguzwa idadi ya mashabiki wanaohudhuria mechi kwenye uwanja wa Wembley, mjini London.
Viongozi hao wawili wamezungumzia pia mahusiano baina ya nchi hizo mbili katika ziara hiyo inayotazamiwa kuwa ya mwisho kwa Kansela Merkel nchini Uingereza kabla ya kuondoka madarakani mwezi Septemba.