Idadi ya raia wanaouawa kutokana na migogoro inazidi kuongezeka nchini Mali, Niger na Burkina Faso, kutokana na mlolongo wa matukio ya mauaji na ulipizaji kisasi.
Hadi kufikia sasa, raia 2,057 wameuawa tangu mwanzoni mwa mwaka 2022, idadi ambayo ni kubwa kuliko 2,021 iliyorekodiwa kwa mwaka mzima wa 2021, ambapo miili iliyopatikana inashuhudiwa kuwa ni mingi kutoka kwa mkusanyiko.
Tangu 2022, kwa kila mwezi kumekuwa na matukio ya mashambulizi hasa katika maeneo ya vijiji ambayo yanashuhudiwa kwa mauaji mengi yanayoongezeka huku ikidaiwa kuwa eneo la Diallassagou katikati mwa Mali raia 132 waliuawa na wengine 86 wakiuawa eneo la Seytenga huko Burkina Faso.
Mwezi Mei mwaka huu, Madjoari – mashariki mwa Burkina Faso, takriban watu 50 waliripotiwa kufariki, idadi inayotajwa kuwa ni kubwa zaidi ya ile ya eneo la Moura katikati mwa Mali ambapo raia 300 waliuawa na jeshi mwezi Machi.
Kwa jumla, kulingana na kituo cha Acled na shirika la Amnesty, raia 11,276 wameuawa katika nchi tatu za Sahelian tangu kuanza kwa mzozo mwaka 2012.
Kati ya mwaka 2012 na 2017, vifo vya raia vilifikia mamia lakini idadi ikaongezeka ghafla hadi kufikia vifo vya raia 1,000 kwa mwaka katika eneo la Sahel pekee.