Wizara ya Ulinzi nchini Burkina-Faso, imemuachilia raia mmoja mwenye asili ya Poland, Bednarski Rafal Kamil ambaye alitekwa nyara kwenye barabara ya Matiakoali-Kantchari Aprili 27, 2022 wakati akielekea nchi ya Niger.

Raia huyo, ambaye ni mwanasiasa aliachiliwa Juni 24 na taarifa zake kutolewa hii leo Juni 30, 2022 ambapo amehamishiwa mji mkuu wa Ouagadougou siku ya Jumanne ambako alikabidhiwa rasmi kwa mamlaka ya Poland ambayo ilituma wajumbe nchini Burkina Faso.

Utekaji nyara wa raia huyo wa Poland, haukuwa umewasilishwa na mamlaka ya Burkinabe hadi kuachiliwa kwake, hali ambayo bado haijafahamika ilitendeka kwa njia zipi ambapo mamlaka za usalama za nchi hiyo zinasema bado zunafuatilia tukio hilo.

Inadaiwa kuwa, matukio ya utekaji nyara umekuwa ukifanyika kwa raia wa kigeni katika miaka ya hivi karibuni nchini Burkina Faso, nchi ambayo imekabiliwa na mashambulizi ya wanajihadi tangu mwaka 2015 na kusababisha maelfu ya watu kupoteza maisha na milioni 1.9 kukimbia makazi yao.

Mapema Desemba 2018, wanandoa wa Italia na Canada walitoweka kwenye barabara kati ya Bobo-Dioulasso na Ouagadougou, na baadaye kuachiliwa huru katika nchi jirani ya Mali baada ya kukaa kifungoni kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Hata hivyo, awali ilidaiwa wanandoa wa Australia Kenneth Elliot na mkewe Jocelyn, walitekwa nyara huko Djibo kaskazini Januari 15, 2016, tukio linalodaiwa kufanywa na kundi la wanajihadi la Ansar Dine.

Idadi ya vifo vya raia yazidi kuongezeka
Utendaji Wakurugenzi, Wakuu wa idara kupimwa