Mipaka ambayo hutenganisha nchi mara nyingi uhalisia wake ni mgumu kuliko mstari unaoonekana kuchorwa kwenye ramani, ambapo ipo mipaka mirefu zaidi kwa nchi zinazopakana na nchi nyingi au nchi zinazopakana na nchi moja pekee au nchi mbili na huenda zisiwe na bahari.

Ugumu huo hutokana na mizozo ya mara kwa mara ambayo hupelekea uwepo wa mahusiano mabovu ya kidiplomasia na mara kadhaa mamlaka zilizo juu yao huchukua hatua za kuwasuluhisha kulingana na aiana ya tatizo linalowafanya kupishana ikiwemo kugombea maeneo, Taifa moja kuingia katika eneo si lake na uvamizi.

Hali hii imepelekea baadhi ya Mataifa kuwa na ujirani mwema na kuelewana bila migogoro ya kimipaka na Mataifa mengine kuwa na uhasama unaosababishwa na mzozo wa kimipaka.

Picha ya Quora

Ifuatayo ni orodha ya nchi 11 ambazo mipaka yake inajulikana kuwa na misukosuko na hatari, na wakati mwingine, haipitiki kutokana na utata kati ya pande mbili zinazokinzana na kufanya ule msemo wa Kiswahili wa ” Mwamba Ngoma huvutia kwake” kuchukua nafasi yake.

  1. Iraq/Iran

Moja ya mipaka hatari zaidi ulimwenguni ni kati ya Iraki na Irani, utata ukitokea katika mto wa Shatt-al-Arab hadi mpaka wa Uturuki, ingawa mpaka huu umetolewa ufafanuzi kwa miaka mingi lakini bado mizozo juu ya eneo hili (hasa matumizi ya mto), imekuwa ikiendelea.

Mwaka wa 1980, Iraq iliishutumu Iran kwa kukalia kwa mabavu ardhi yake kinyume cha sheria na ilirusha makombora kadhaa kuwarudisha nyuma na miaka nane baadaye, nchi hizo mbili zilitia saini azimio la amani la Umoja wa Mataifa, lakini hata hivyo hiyo haijasaidia kwani mpaka leo bado hawajaacha kupigana na mashambulizi ya kuvuka mpaka yameendelea.

Picha ya Quora

  1. Pakistan/Afghanistan

Mpaka kati ya Pakistani na Afghanistan unaitwa Mstari wa Durand, ukiwa una urefu wa maili 1,510. Migogoro baina ya pande hizi mbili ni ya miaka mingi na katika siku za hivi karibuni, mpaka huu ulipingwa na Taliban na baadaye rais wa Afghanistan mwaka 2001 naye akaupinga.

Mwaka 2003, vikosi vya jeshi kutoka pande zote mbili vilihusika katika mapigano ya kivita na miaka minne baadaye, Pakistan ilianza kujenga uzio kama njia ya kuwazuia wanamgambo wa Taliban kuvuka.

Hatari iliyopo hapa ni mbinu za udhibiti wa serikali zote mbili huku watu kila upande ukiwa umebeba silaha, uwepo wa magendo, mauaji na utekaji nyara haramu ni vitu vya kawaida katika mpaka huu na hivi karibuni, barabara kuu inayounganisha nchi hizo mbili ilifungwa kutokana na kutoelewana kuhusu lango lililojengwa na Pakistani.

Hata hivyo, mzozo huo ulimalizwa kwa mtutu wa Bunduki na mirindimo ya risasi na ulisababisha vifo vya watu watatu na wengine 24 kujeruhiwa.

Picha ya Future Travel.

  1. Uchina/Korea Kaskazini

Uchina na Korea Kaskazini zimetenganishwa na mito miwili, Tumen na Yalu, na milima ya Paektu. Mpaka huu una usalama duni na unapokea watu wengi wanaoikimbia Korea Kaskazini ambapo katika miaka kumi iliyopita, nchi zote mbili zilianza kujenga uzio na kuta.

Tangu kuanza kwa utawala wa Kim Jong-Il na kuongezeka kwa wahamiaji wa Korea Kaskazini nchini China, mizozo ya maeneo imekuwa ni ya kawaida na yenye kuleta wasiwasi. Pia kumekuwa na ripoti za wanajeshi wa Korea Kaskazini kuvuka mpaka na kuiba chakula na pesa huku maafisa wa ngazi ya chini wakipokea mgao mdogo wa chakula.

Aprili 2016, China ilipeleka karibu wanajeshi 2,000 kwenye mpaka baada ya ripoti kwamba Pyongyang inapanga majaribio ya nyuklia ambapo Uchina ilithibitisha kuwa raia wake watatu wa waliuawa kwenye mpaka huo, huku ikisema uchunguzi ulikiwa ukiendelea ili kubaini ukweli.

Picha ya AFP.

  1. Colombia/Ecuador

Mizozo kati ya Colombia na Ecuador imeongezeka katika miaka ya hivi karibuni kutokana na kundi la waasi la Colombia linalojulikana kama Mapinduzi ya Jeshi la Colombia (Jeshi la Wananchi au FARC). Kwa nyakati tofauti, serikali ya Colombia imetuma wanajeshi wake katika ardhi ya Ecuador ikiwa ni jaribio la kushambulia kundi hilo.

Wanachama wa FARC ambao ni kundi la vurugu kupita kiasi wamevamia ardhi kando ya mpaka huo na kwa kutumia chokaa na mabomu ya ardhini ambayo yamewalazimisha maelfu ya watu wa kiasili kuondoka katika ardhi ya makabila yao. Pia kundi hili linahusika na mauaji ya zaidi ya watu 200,000 katika miaka hamsini iliyopita.

Hata hivyo, viwango vya mauaji ya hivi majuzi katika miji ya mpakani vimefikia watu 96 kwa kila watu 100,000. Rais wa Ecuador alisema wanajeshi wa Colombia hawakuwa na ruhusa ya kuvuka mpaka na wameishutumu Ecuador kwa kuwahifadhi magaidi na Ecuador tangu wakati huo imeongeza juhudi za kuwaondoa FARC.

Picha ya Caracol Radio.

  1. Niger/Chad

Moja ya maeneo yenye makundi mabaya zaidi ya kigaidi duniani, uasi wa Boko Haram unapatikana kwenye mpaka wa Niger-Chad. Ili kupambana na kundi hili, Chad imetuma wanajeshi 2,000 katika mji wa mpakani uliopo Bosso, upande wa Niger.

Ghasia katika mji huu zimepelekea zaidi ya watu 17,000 kukimbia eneo hilo na tangu kuwasili kwa wanajeshi hao, wanajeshi 32 (30 kutoka Chad na 2), kutoka Niger na magaidi 55 wamepoteza maisha na hata hivyo nchi hizi mbili zimekuwa na operesheni za pamoja za kijeshi tangu mwanzoni mwa mwaka 2015.

  1. Yemen/Saudi Arabia

Mpaka huu una urefu wa maili 1,100 kati ya Yemen na Saudi Arabia, ukiwa umeshuhudia viwango vya juu sana vya vurugu. Nchi hizo mbili zimekumbwa na mzozo mkali kwa miaka 65 iliyopita. Saudi Arabia imekuwa na ongezeko la silaha za magendo, magaidi wa Al Qaeda, na wakimbizi wa kiuchumi (kutoka Ethiopia, Yemen, na Somalia), hali iliyosababisha Serikali kujenga ukuta.

Picha ya Arizona Daily Star.

Yemen inapinga kizuizi hicho, ikisema kinakiuka haki za malisho ya wachungaji. Nchi hizo mbili zimekuwa katika vita rasmi tangu Machi 2015 na takriban raia na wanajeshi 6,000 wameuawa tangu kuanza kwa vita hivyo huku kwa siku moja pekee, makombora 15 – 130 yanarushwa hadi Saudi Arabia.

  1. Bangladesh/India

Bangladesh na India zina mpaka wenye urefu wa maili 2,545, huu ni mojawapo wa mpaka mrefu zaidi duniani. Mpaka huo ni mgumu na unajumuisha maeneo yenye kutatanisha, wakati mwingine ardhi ya Wahindi iliyozungukwa na eneo la Bangladeshi ndani ya eneo la Wahindi! Ni njia ya kawaida kwa bidhaa za magendo kutoka India hadi Bangladesh na wahamiaji wasio na vibali kutoka Bangladesh hadi India.

Kutokana na viwango vya juu vya uhamiaji, Vikosi vya Usalama vya Mipakani vya India vimeamua kuwa na sera ya maono ingawa wakati mwingine, “vivukio haramu” ni matokeo yasiyo rasmi na yenye kuifanya njia kuwa ngumu zaidi mpakani katika jaribio la kufikia eneo tofauti la Bangladeshi. Sera hii ya kuua kwa macho imesababisha zaidi ya vifo 1,000 kati ya mwaka 2000 na 2010.

Picha ya Theworld.org

  1. Mexico/Marekani

Mpaka wa Mexico na Marekani huanzia California hadi Texas kwa jumla ya maili 1,989, na una idadi kubwa zaidi ya vivuko halali vya kila mwaka ulimwenguni. mpaka huu unapita karibu na maeneo makubwa ya mijini na juu ya majangwa yenye ukiwa. Takriban maajenti 20,000 wa doria mpakani wamekusanyika kuzunguka miji mikubwa na kuacha jangwa bila ulinzi.

Hii hufanya uwepo wa watu 500,000 wanaojaribu kuvuka mpaka kinyume cha sheria hadi jangwani ambapo mamia kadhaa hufa kila mwaka na eneo hilo ni hatari sana katika eneo la El Paso-Juarez ambalo linajulikana kwa walanguzi wa mihadarati.

Mihadarati hiyo, husafirisha kama au pamoja na dawa nyingine za kulevya kwa ulinzi mkali wa silaha na watu kwenye mpaka. Mamia ya watu wamekufa hapa baada ya mapigano kati ya Polisi na vikundi au magenge ya wahalifu na vurugu hizo zimeenea katika maeneo mengine ya Amerika.

Picha ya Quora.

  1. Israeli/Syria

Mzozo wa mpaka kati ya Israel na Syria ulianza miaka mingi iliyopita, mwanzoni mwa miaka ya 1920, Uingereza ilichora mipaka ikitoa upande wa Syria kwa Ufaransa. Kisha tena baadaye kujumuisha Miinuko ya Golan.

Eneo hili limekuwa na ushindani mkubwa kwa karibu miaka 100 na nchi hizo mbili zimekuwa kwenye vita mara kadhaa zikichukua udhibiti wa vipande mbalimbali vya ardhi. Leo, mpaka huu umekuwa ni eneo la vita la moja kwa moja, na risasi zikirusha kutoka pande zote mbili hata hivyo, ghasia zimeongezeka tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria kuanza.

  1. India/Pakistani

Mpaka wa India na Pakistani ni maili 1,800 za ardhi yenye ulinzi mkali na hatari sana. mpaka huu umelindwa sana na ndio mpaka pekee unaoonekana kutoka angani kutokana na taa za mafuriko ya volteji ya juu upande wa India.

Picha ya Top10ish.

Tangu mgawanyiko wa mwaka 1947 ambao ulishuhudia mamia kwa maelfu ya watu wakipoteza maisha. Nchi hizi zimepigana katika vita vingine vitatu na kutumia angalau miaka 25 kupinga madai ya jimbo la Kashmir na barafu ya mlima. Idadi ya waliojeruhiwa imepita alama ya maisha 50,000.

  1. Korea Kusini/Korea Kaskazini

Ni eneo lisilo na Kijeshi la Korea (DMZ), ukiwa ni mpaka wa maili 160 kati ya Korea Kaskazini na Kusini. Eneo hili linalindwa sana na askari wa pande zote mbili na limekamilika kwa waya wa miinuko na mabomu ya ardhini yanayotumika.

Mwisho wa Vita vya Korea haukufanya chochote kumaliza uhasama kati ya mataifa hayo mawili, kwani wamekuwa wakipigana kwa zaidi ya miaka 60 na hawatambui hadhi ya uhuru wa kila mmoja.

Mamia ya watu wamekufa katika mazingira haya ya wasiwasi, wakiwemo raia wa Marekani ambapo mvutano wa mataifa haya ni mzito sana Na DMZ iliundwa kama aina ya eneo la bafa, ili kuweka nchi na vikosi vyao vya kijeshi katika umbali salama, kutoka kwa kila mmoja na yeyote anayejaribu kuvuka mstari atapigwa risasi.

Makamu wa Rais aiasa jamii malezi mema ya Vijana
Wanane wafariki kwa mashambulizi ya risasi