UZEMBE WA KUFIKIRI, Watu wengi wanaoamini kuwepo kwa matukio ya bahati mbaya katika maisha wanaelezwa na wataalamu kuwa na kasoro katika upeo wa kufikiri. Hivyo inashauriwa kuwa mtu anayetaka kuepukana na bahati mbaya lazima awe hai katika fikra, hasa upataji wa jibu la mapema juu ya nini kitatokea katika kutenda kwake.
KUTOTUMIA UWEZO WOTE, Mwanadamu anatajwa kuwa na uwezo mkubwa sana wa kufanya mambo kuliko wengi wao wanavyodhani. Wahanga wengi wa bahati mbaya ni wale ambao hawatumii uwezo wao wote au zaidi ya nusu ya vipaji vyao katika kupambana na matokeo mabaya.
KUAMINI VIASHIRIA VYA KUSHINDWA, Kuna watu ambao hupatwa na matokeo ya bahati mbaya baada ya kuamini viashiria vya kushindwa na kuacha kujizatiti katika nguvu za ushindi.
KUYUMBA KATIKA MAAMUZI, Kuna watu ambao kwa hakika kabisa wanaweza kuwa wamefikiri vema, wametumia uwezo wao wote, hawakuamini viashiria, lakini wakajikuta wanapatwa na bahati mbaya kwa kuyumba katika maamuzi, hasa wakati wa kuhitimisha jambo fulani.
KUMBUKUMBU MBAYA, Katika maisha yetu kuna watu wengi ambao wanasogeza bahati mbaya kwa kujaza kumbukumbu mbaya za matukio hasi kwenye akili zao.Wingi wa kumbukumbu mbaya ni kosa kubwa kwani hutengeneza uzembe wa mwili ambao huleta matokeo mabaya bila mhusika kujijua.